GET /api/v0.1/hansard/entries/32885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 32885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/32885/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Otuoma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 132,
        "legal_name": "Paul Nyongesa Otuoma",
        "slug": "paul-otuoma"
    },
    "content": "Ahsante. Bwana Naibu Spika wa Muda ameniambia nichague, na mimi nimechagua Kiswahili. Kuhusu vijana wa Samburu ambao wanahusika na ufugaji wa ng’ombe, mpango wa youth polytechnics utasambazwa katika kila maeneo ya ubunge. Kuna sehemu ambazo zilikuwa na polytechnics nyingi kuliko sehemu zingine. Katika sehemu ambazo hazina, tunajaribu kutumia mpango wa affirmative action ili kuziwezesha kuwa na youth polytechnics. Katika youth polytechnics, kuna programmes ambazo zimewekwa ambazo zinalenga vijana wanaotoka eneo kama hilo. Kama wangependa kujifunza jinsi ya kuendesha biashara, mipango itawekwa kulingana na hayo. Kama wanataka fedha ili waweze kuendesha biashara yao, mikakati itawekwa kulingana na matarajio yao. Kitu cha muhimu ni kuwahimiza Wabunge kwamba, katika wakati huu tunaposajili youth polytechnics--- Ikiwa kuna eneo halina, huu ni muda mzuri wa kuja kwetu, kufuatilia na kujua ni youth polytechnics gani ambazo zimewekwa katika mipango ya Serikali. Kama kuna zile ambazo hazijawekwa, itakuwa vizuri ukituletea kupitia kwa Youth Development Officer na DDC ili tujue ni zipi tutaweza kusajili. Nafikiri hilo ni jukumu kubwa la waakilishi wa wananchi."
}