GET /api/v0.1/hansard/entries/328860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 328860,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/328860/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kuttuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika Wa Muda ninashukuru. Mkuu wa Sheria amezugumzia uhusiano wa Kenya na Tanzania; kwamba ni wa chanda na pete, na kwamba wanashirikiana bega kwa bega, lakini ila ya hayo yote, hajapata kutatua matatizo ya hao Wakenya ambao wako mbaroni. Familia ya hawa watu wanalia usiku kucha. Ni hatua zipi ambazo serikali inachukua kuhakikisha kwamba hawa Wakenya wamerejeshwa humu nchini wakafanyiwe uchunguzi na sheria ifuate mkondo wake? Na kwa majibu yake, si maajabu kwamba taifa la Kenya limekuwa na uzoefu wa kupeana wakenya kufanyiwa kesi nje ikiwemo sasa washukiwa wanne wa vita vya kisiasa. Na hii inanifanya kuingiwa na wasiwasi kusema wale wale wajiokoe na wasiachie mwingine aje kuwaokoa."
}