GET /api/v0.1/hansard/entries/330165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 330165,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330165/?format=api",
    "text_counter": 328,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Baiya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 8,
        "legal_name": "Peter Njoroge Baiya",
        "slug": "peter-baiya"
    },
    "content": "Bw. Spika, wingi wa vituo vya kuandikisha watu ambavyo ni vya kuhamahama vinategemea ukubwa wa sehemu hiyo sio wingi wa watu peke yake. Lakini kama sehemu ni pana na watu wanaenda safari ndefu kufika kwa ofisi, sehemu kama hizo tutazipatia vituo kama hivi. Kwa hivyo, siwezi kusema ni vingapi kwa kila wilaya. Pengine ukiniuliza wilaya fulani vitakuwa vingapi, ninaweza kufanya utafiti na nitakujibu."
}