GET /api/v0.1/hansard/entries/330885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 330885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330885/?format=api",
    "text_counter": 1048,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Ahsante sana Bwana Naibu Spika. Pia naunga mkono Hoja hii ya sisi kufunga ili kuelekea maeneo ya Bunge tulikotoka; kule tulikochaguliwa. Kazi imefanyika na Wabunge sasa hivi wanatakiwa kuelekea manyumbani ili waweze kuzungumza na wananchi waliotupatia fursa hii ya kuwa kwenye Bunge hili la kifahari, Bunge la Kumi. Ningependa pia kuchukua fursa hii kuwapongeza Bwana Nyegenye na Bwana Bundi kwa kuwa wameteuliwa kusimamia ukatibu wa Bunge na Senate. Wataanza kazi hivi karibuni ili kutekeleza majukumu hayo ambayo ni mazito. Kwa sababu ni watu ambao walikuwa wameshafanya kazi na wanaelewa kazi za hapa, itakuwa nyepesi kwao. Natumaini kwamba wataweza kuiendeleza kazi nzuri ambayo ilifanywa na Bwana Patrick Gichohi ambaye anastaafu baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi hapa Bungeni. Wabunge wa Bunge hili la Kumi wamefanya kazi nyingi sana. Tunapoelekea nyumbani, sasa hivi ni wakati wa kuenda kuhakikisha kwamba shughuli za kimaendeleo"
}