GET /api/v0.1/hansard/entries/330887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 330887,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330887/?format=api",
    "text_counter": 1050,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kule mashinani zinaendelezwa vizuri. Ningependa pia tuchukue nafasi hii kuzungumzia siasa ambazo ni za kuwaunganisha Wakenya. Vile vile, tuzungumze siasa ambazo si za chuki na kuwaunganisha Wakenya hasa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu unaokuja mwezi wa tatu mwaka ujao. Ningependa kuunga mkono Hoja hii wakati huu tukielekea manyumbani na mashinani ili tukirudi hapa, tumalizie mkondo wa mwisho wa Bunge hili la Kumi na turudi tena ili tuwaulize wananchi fursa ya kurudi kufanya kazi tena kama watatuona tukiwa tunafaa. Wakenya wako tayari baada ya kuwa na Katiba mpya ili kuona uchaguzi unaokuja umefanywa kwa njia nzuri ili wapate mafanikio yaliyo katika Katiba mpya. Pia, ningependa kuwapongeza Makamishina wetu wa hapa Bunge ambao wamefanya kazi nzuri ya kuwapa nafasi wafanyikazi wetu wakiwa hapo ndani na haswa wamama ambao wamechukua asilimia 40. Haikuwa rahisi kwao kuipanga na kuipangua ili watoshee hapo, ijapokuwa najua walifanya kazi nzuri katika mtihani waliofanya, walipita na alama za juu sana. Naunga mkono Hoja hii."
}