GET /api/v0.1/hansard/entries/330888/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 330888,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330888/?format=api",
    "text_counter": 1051,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bwana Naibu wa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono Hoja hii. Hii ni Hoja ya likizo ambayo ilibisha hodi na imeingia wakati unaofaa. Likizo hii itatupa nafasi nzuri ya kurudi nyumbani na kufanya kazi hasa tukitumia pesa za CDF. Pesa za CDF, imesemakana tutapewa asilimia 50. Hiyo imeshaingia na sasa tunangoja asilimia 50. Itakapofika mwezi wa Januari na pesa ziwe hazijatumika, zinaweza kuitishwa tena. Kwa hivyo, tutapata nafasi ya kuweza kuzitumia ili tuweze kuwafanyia wananchi maendeleo. Bw. Naibu wa Spika, jambo lingine ni kwamba, ningependa kuiomba Serikali kwa dhati, tunapoelekea kwenye mfumo mpya wa serikali za kaunti; uchaguzi utafanywa tarehe 4 Machi, 2013. Mwezi mmoja baadaye, tutakuwa tumeweka watu katika sehemu zinazofaa ili waweze kuhudumu. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba huenda kukawa hakuna makao ya kufanyia vikao vya bunge za kaunti. Kwa hivyo, ningependa Serikali ilizingatie suala hili na kuhakikisha kwamba pesa za kutosha zimetengwa ili kujenga ofisi na majengo ya bunge za kaunti ili ziweze kutafakari juu ya mahitaji ya wananchi. Jambo lingine ambalo ningependa kuligusia tunapoelekea likizoni ni kwamba kuna umuhimu wa kujaribu kuwaunganisha Wakenya. Siaza za ukabila zimeenea kote nchini. Ukiangalia utaona kwamba Wakenya katika maeneo yote humu nchini wameshikana na watu wa sehemu hizo. Wakenya wanajiuliza iwapo tuna viongozi ambao wanaweze kujitolea na kuiongoza nchi hii, wakizingatia maslahi ya taifa lote. Kila mtu anapozungumza, utaona kwamba waliosimama nyuma yake ni watu kutoka kwa kabila lake, ambao wanamwambia kwamba yeye tu ndiye anayefaa kuitawala nchi hii. Bw. Naibu wa Spika, maombi ni kuona kwamba tumekuwa na mhe. Jomo Kenyatta mwingine, ambaye aliunganisha taifa hili. Wakati kulipokuwa na mgawanyiko mkubwa katika nchi hii, Daniel arap Moi na Ronald Ngala wakiwa katika chama cha KADU, na Paul Ng’ei akiwa APP, Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa Rais wa taifa hili, hakuwangojea watu hao waende kwake. Aliwatafuta, akawaweka pamoja na kuliunganisha taifa hili, pamoja na hayati Jaramogi Oginga Odinga. Katika taifa hili, bado ninamtafuta mtu mwenye hekima kama hayata Jomo Kenyatta. Vile vile, mstaafu Rais Moi pia alijaribu kuwaunganisha Wakenya. Sasa ninaomba tuwe na watu kama hao, ambao wanaweza kuwaunganisha Wakenya ili tuweze kwenda mbele."
}