GET /api/v0.1/hansard/entries/330893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 330893,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330893/?format=api",
    "text_counter": 1056,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, asante sana kwa nafasi hii umenipa. Niko na machache sana. Kwanza nashukuru Kamati ya Huduma ya Bunge, Parliamentary Service Commission, kwa kazi nzuri ambayo wamefanya. Leo tuna Bunge la kifahari. Tunaketi kwa viti vizuri, tuna Bunge lipya ambalo limefanyiwa ukarabati na tunajivunia. Aisifuye mvua imemnyea na hiyo ndio sifa. Leo nashukuru pia kwa kazi ambayo wamefanya kuteua wale walio na tajiriba ya miaka mingi katika sheria kuwa makatibu wa Bunge. Bw. Naibu Spika niruhusu niwapatie changamoto wale ambao wanaenda kuwa makatibu. Bunge hili lina Wabunge ambao wamejitolea lakini wana changamoto ya kushughulikia maslahi ya wafanyakazi wa Bunge hili ili isiwe ni Bunge ambalo Wabunge wanajivunia lakini wafanyakazi wanavumilia. Waangalie maslahi ya wafanyakazi wa Bunge, watu wa chini kwa mishahara yao na hali yao. Katika Bunge hili tunahitaji usafi. Unapoketi kwenye ukumbi wa Bunge, masaa kama haya utapata kwamba mbu ni tele na wavamia walioko kule wakisherehekea. Sisi tumekuwa mlo wa mbu tunapoketi kwenye ukumbi. Tungependa kamati ambayo inashughulikia maslahi ya Wabunge ichukue hatua ya kuweza kuimairisha maeneo hayo. Nikikamilizia, ningependa kusema kwamba usalama wa taifa ni kitu ambacho kinatakikana kupewa kipaumbele. Kwa sasa usalama umezorota na kama tunakwenda"
}