GET /api/v0.1/hansard/entries/330895/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 330895,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/330895/?format=api",
"text_counter": 1058,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "likizo Bunge ndio imekuwa macho na imekuwa mnyapara wa Serikali ili iweke mikakati ya kuimarisha usalama. Tungependa Serikali iweke mikakati ya kutosha. Nikikamilisha, ningependa kuomba kamati ambayo inahusika na shughuli za Bunge, nimemuona Kiranja wa Serikali yuko hapa na tutakaporejea, tuna Miswada muhimu kama ule ambao mimi nimeuleta Bungeni wa kusindikiza Serikali kwamba baada ya vijana kukamilisha masomo yao katika vyuo, Serikali iwape nafasi ya kupata ujuzi kwa miaka mitatu ili wanapotafuta kazi isiwe kwamba hawana tajiriba ya miaka miwili ama mitatu. Narudia tena, kwamba naomba wakati tutakaporejelea vikao vya Bunge, tafadhali Mswada huo upewe kipaumbele ili vijana waweze kupata nafasi ya kuhudumu kwa muda wanapotafuta nafasi za kazi. Kwa hayo nawatakia heri na fanaka mnapoingia katika ulingo wa siasa wa mwisho. Itategemea ukali wa meno na urefu wa kucha. Asante Bw. Naibu Spika, na mlale unono."
}