GET /api/v0.1/hansard/entries/33141/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33141,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33141/?format=api",
    "text_counter": 387,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Assistant Minister for Education (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mr. Mwatela): Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Waziri M. Kilonzo, ambaye anafanya kazi yake kwa bidii sana, kwa kuleta Mswada huu ambao, bila shaka, tutaupitisha kuwa sheria. Bw. Naibu Spika wa Muda, sikumbuki ni mwaka upi, lakini utakumbuka nilikuja kukuona hospitali ukiwa umefungwa pingu na umefungiwa kwenye kitanda, tukiwa na jirani yako, Dr. Kiriti. Hali hiyo ni ya kudunisha ubinadamu. Mswada huu ni kama kilele cha vita dhidi ya kukosa heshima kwa utu. Ninaunga mkono wale ambao walitangulia kuzungumza, lakini pia ningetaka kuongeza kuwa wengi waliochangia sana katika kufikia hali hii ni watu wa hali ya chini kimasomo ambao walijitolea. Walikuwa akina mama na hata vijana. Wakati tunaposema kuwa ni lazima mtu awe na shahada ya chuo kikuu ndio aketi kwenye Tume hii, haifai. Wakati wa kupigana hivi vita, tulikuwa"
}