GET /api/v0.1/hansard/entries/33144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33144/?format=api",
    "text_counter": 390,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tukitumia kila mtu lakini wakati tunapounda Tume hii, tunawaweka nje. Ningemuomba Waziri aangalie sehemu hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kweli tunahitaji watu walio na uwezo wa kuelewa mambo, lakini shahada ya chuo kikuu haiwezi kuwa ni lazima. Inawezekana kabisa kuwa mtu wa kawaida tu ambaye amesoma mpaka sekondari lakini ametumika kikamilifu kupigania haki hizi. Kwa hivyo, tuangalie sana mahitaji ambayo tunayaweka ili tusije tukawaweka watu wetu ambao walijishughulisha sana kutafuta hali hii nje. Ningeomba kuwa wakati tunapoangazia matakwa mengine, tuhakikishe kuwa tumehusisha jamii yote ili tuwe na upande wa vijana, wazee na akina mama. Tutakapounda Tume hii, iwakilishe jamii kwa jumla. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}