GET /api/v0.1/hansard/entries/331490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 331490,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/331490/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Spika ningependa kuitisha taarifa kutoka kwa Wizara ya Kilimo. Katika Taarifa yake, ningependa Waziri aeleze mambo yafuatayo:- (i) Serikali inatarajia kiasi gani cha mahindi kuvunwa mwaka huu? (ii) Serikali imetenga pesa ngapi katika makadirio ya Bajeti mwaka huu kwa ununuzi wa mahindi kupitia halimashauri ya nafaka ya taifa? (iii) Serikali itanunua kwa pesa ngapi gunia moja ya kilo tisini ya mahindi kupitia kwa halimashauri ya nafaka ya taifa. (iv) Je, Waziri ana habari kwamba kuna mvua ya El Nino ambayo imeongeza unyevu na baridi kwa mahindi? Ni hatua gani Serikali imeweka kupunguzia wakulima hasara kwa hali hii mbaya ya anga wakati huu wa mavuno?"
}