GET /api/v0.1/hansard/entries/331613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 331613,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/331613/?format=api",
"text_counter": 331,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Yangu ni kuunga mkono marekebisho ya sheria hii. Kulitokea makosa kwetu sisi kuchukua majukumu ya bodi ya kukagua majaji na mahakimu na kugawanya majukumu ili mahakimu waweze kukaguliwa na tume ya mahakama ambayo ilikuwa na shughuli na kazi tofauti ambazo ziliwekwa kisheria kwenye Katiba kwa mujibu wa Katiba yetu ya Kenya. Jambo hili limetatiza sana hasa Wakenya ambao walitaka kazi hii iendelee vilivyo na ilivyopaswa ili majaji na mahakimu waweze kuendelea na kazi zao bila wasiwasi. Kwa hivyo, bodi hii ni haki kabisa irudishiwe majukumu yake iweze kufanya kazi hii na vile vile Waziri ambaye anasimamia maswala ya haki hapa nchini aweze kuhakikisha ya kwamba wanaharakisha kazi ijapokuwa wameweza kuwekewa vikwazo, waweze kutekeleza kazi hii. Bodi hii ya ukaguzi ni ya kipekee ulimwengu mzima. Tumepata sifa sana kwa kazi nzuri ambayo wanafanya na vile vile kuwawezesha kufanya kazi bila hali ya wasiwasi. Ninaunga mkono marekebisho haya yaweze kutekelezwa mara moja. Asante sana."
}