GET /api/v0.1/hansard/entries/3318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 3318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/3318/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kimunya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 174,
        "legal_name": "Amos Muhinga Kimunya",
        "slug": "amos-kimunya"
    },
    "content": "Ningependa kuarifu Bunge hili kuwa magari yote yanayoingizwa hapa nchini kupitia Bandari ya Mombasa hulipiwa ushuru. Ni baada ya kulipa ushuru ndio unapewa nafasi ya kutueleza unataka kuitumia gari yako kwa njia ipi. Ikiwa unataka kufanya biashara ya matatu kwa kutumia gari ndogo kama Nissan au inayobeba watu 14, unanyimwa leseni. Hii ni kwa sababu Serikali wakati huu haitoi leseni kwa watu wanaotaka kufanya biashara ya matatu wakitumia magari inayobeba abiria 14. Sheria za uchukuzi wa umma hairuhusu magari yanayobeba chini ya watu 14."
}