GET /api/v0.1/hansard/entries/33185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 33185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33185/?format=api",
"text_counter": 431,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii ili pia niweze kuchangia Mswada huu muhimu sana. Nitaanza kwa kusema kuwa ninaunga mkono kwa dhati sheria hii pendekezi ya kubuni tume ambayo ndiyo itakuwa mlinzi, au bawabu, wa haki za kibinadumu na wananchi wa taifa hili tukufu la Kenya. Ningependa kumshukuru sana Waziri was Haki, Utangamano wa Kitaifa na Maswala ya Kikatiba, mhe Mutula Kilonzo, kwa harakati zote ambazo amechukua kuhakikisha kuwa shughuli hii ya kutekeleza Katiba hii mpya inaenda kwa kasi inayostahili. Ni vyema Wakenya wafahamu kuwa utekelezaji wa Katiba si swala rahisi kwa sababu tumo kwenye shughuli ya kubadili misingi ya taifa hili."
}