GET /api/v0.1/hansard/entries/33188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 33188,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33188/?format=api",
"text_counter": 434,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, historia inatufunza kuwa hakuna jamii yoyote inayoendelea ikiwa ni jamii ambayo hailindi na haichungi kwa uangalifu sana maslahi ya wananchi wake. Katika mazingira ya dhuluma na ukandamizaji wa haki za kibinadamu, hakuna maendeleo yanayowezekana. Hata maswala ya umoja, amani na utulivu hayawezekani katika mazingira ya dhuluma. Hatuwezi kuwa jamii iliyo na umoja, usawa na amani ikiwa sisi ni jamii ambayo haitazami kwa makini haki za kila moja wetu. Jamii yetu ya Kenya ni jamii ambayo imekuwa na historia ya dhuluma. Imekuwa na historia ya ukandamizaji wa haki za wananchi wa taifa hili. Kumekuwa na mauji ya kiholela. Ukitazama historia ya taifa hili, kuna Wakenya ambao wamepoteza maisha yao. Ukitazama historia ya taifa hili tangu tupate Uhuru, utapata kwamba kumekuwa na mauaji ambayo mpaka leo hatujajua chanzo chake na hatujapata jibu. Akina Tom Mboya, J.M. Kariuki, Robert Ouko na Odhiambo Mbai. Hawa ni Wakenya ambao walipoteza maisha yao kwa njia ya kiholela kutokana na dhuluma na ukandamizaji wa haki za wananchi wa taifa hili. Swala hili limekera taifa hili tangu tupate Uhuru."
}