GET /api/v0.1/hansard/entries/33193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33193,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33193/?format=api",
    "text_counter": 439,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ya kuweza kuhakikisha kwamba Tume hii imejikita katika misingi ya kikatiba. Kwa hivyo, itakuwa mlinzi wa haki za kila Mkenya. Tume hii itatupa fursa ya kuzika katika kaburi la sahau historia yetu ya dhuluma na ukandamizaji wa haki za Mkenya yeyote. Swala la mauaji ya kiholela na kikatili ni mambo ambayo tunataka kuyazika katika kaburi la sahau. Hatutaki kushuhudia mambo kama haya tena katika taifa hili la Kenya. Mimi ninaunga mkono kubuniwa kwa Tume hii. Nina imani kwamba ikiwa Tume hii itapewa nafasi na rasilmali za kutosha na itafanya kazi vilivyo. Swala hili la rasilmali ni changamoto kwa Serikali yetu hii ya mseto na serikali zitakazokuja hapo mbeleni. Ni lazima Tume hii ipewe rasilmili za kutosha ili itekeleze majukumu yake. Majukumu ya kuhakikisha ya kwamba haki ya kila Mkenya inalindwa kwa dhati. Sura ya 4 ya Katiba mpya ni msingi wa haki za kila Mkenya hapa nchini. Sura hii imeeleza haki za kila aina; haki za kisiasa, kiuchumi, kimazingira, kijinsia na kadhalika. Ni furaha yangu kuona ya kwamba haki zote zimelindwa katika sura hii ya Katiba. Itakuwa ni jukumu la Tume hii kuhakikisha ya kwamba haki zote zinaheshimiwa kuambatana na Katiba yetu. Tume hii itashughulikia haki za kila Mkenya awe anaishi Budalangi, Kinango, Wajir, Tondonyang na kwingineko. Tunajua ya kwamba baada ya miaka 50 ya Uhuru kuna Wakenya ambao hawana usalama. Haya ni maswala ambao tunashuhudia katika Kenya huru. Muda mfupi uliopita, tulijadili katika Bunge hili mauaji ya zaidi Wakenya 50 kule Tudonyang katika Kaunti ya Turkana. Hawa ni Wakenya ambao waliuwawa kiholela. Wiki mbili zilizopita, mauaji mengine kama haya yalitokea kule Todonyang. Huu ni ukiukaji wa haki za kibinadamu. Tunajua jukumu muhimu zaidi ya serikali yeyote ni kuhakikisha ya kwamba kila mwananchi ana usalama wa kutosha. Ni jukumu la Serikali kulinda mali na uhai wa kila Mkenya kwa dhati. Tunajadili jambo hili wakati zaidi ya Wakenya milioni nne wamekumbwa na baa la njaa. Hilo ni swala la haki za kibinadamu. Ningependa Serikali yetu ifahamu kwamba hata tunapobuni Tume hii ya haki za kibinadamu, tayari haki za kibinadamu za Wakenya wengi zinakiukwa. Tutakuaje taifa huru; taifa ambalo linapiga hatua za maendeleo na kwamba ifikiapo mwaka wa 2030 tutakuwa tumefikia kiwango kikubwa cha maendeleo, ikiwa hatuwezi kuwalisha wananchi wetu? Sura ya 4 ya Katiba yetu inasema kwamba kila Mkenya ana haki ya kupata chakula na kuishi vizuri. Hii ni changamoto kubwa kwa Serikali kuwa hata wakati huu tunapobuni Tume hizi tuwe na sera ya kuhakikisha ya kwamba Wakenya wanavuna matunda ya haki zote katika sura hii ya Katiba mpya. Ningependa kuhimiza Serikali hii wakati huu wa kujenga Kenya upya, isingojee kesho wala kesho kutwa kuchukua hatua itakayotupeleka mbele. Ni lazima Serikali hii ichukue kila hatua inayowezekana kuhakikisha ya kwamba Wakenya wanapata chakula cha kutosha, vyombo vya habari vinahudumu katika mazingira ya uwazi, haki, usawa na bila ukandamizaji. Tumeshuhudia hapo mbeleni mashumbulizi kwa vyombo vya habari. Miaka mitano iliopita kulikuwa na kisa cha kuaibisha katika taifa hili. Wakati ambao majambazi walishambulia ofisi za gazeti la The Standard hapa Nairobi. Hadi kufikia sasa, Serikali haijawaeleza Wakenya ni akina hawa walioshambulia ofisi hizo. Ni akina nani hawa waliokuwa majasusi wa dhuluma ambao walichukua hatua za kukandamiza haki za vyombo vya habari? Uwazi wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari ni mojawapo ya haki muhimu zaidi katika Sura ya 4 ya Katiba yetu. Na hili ni swala ambalo"
}