GET /api/v0.1/hansard/entries/33196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 33196,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33196/?format=api",
"text_counter": 442,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tume hii itapata fursa ya kulishughulikia na kuhakikisha kwamba haki hii inalindwa kikamilifu. Bw. Naibu Spika wa Muda, taifa hili halitapata utulivu kamili ikiwa hatutatua dhuluma za kihistoria. Mhe. Chachu alipokuwa anachangia Hoja hii, alizungumuzia mauaji ya kiholela ambayo yameshuhudiwa katika taifa hili katika sehemu mbalimbali. Haya ni mauaji ambayo hatujawahi kuambiwa yalifanywa na akina nani, yalisababishwa na nini na haki kwa wahasiriwa itapatikana lini. Na hata muaaji ya Wakenya mashuhuri kwa vile Tom Mboya, J.M. Kariuki, Robert Ouko, Odhiambo Mbai na wengine, hatujawahi kuelezwa yalisababishwa na akina nani. Taifa hili halitapata utulivu mpaka tutakapoeleza kwa uwazi ni nani waliyotekeleza mauaji hayo na kutatua dhuluma zote za kihistoria. Tumekuwa na muda ambao hata waheshimiwa Wabunge hapa Bungeni hawakuwa na uhuru wa kujieleza. Kumekuwa na wakati ambao Wabunge wamewahi kutiwa mbaroni katika majengo haya ya Bunge kinyume cha sheria. Ni hizo ni dhuluma za kihistoria ambazo mpaka wakati ambao tutazishughulikia na tuhakikishe ya kwamba hazirudiwi tena, hapo ndipo basi tutakapokuwa tumefika katika hali ya utulivu wa kitaifa. Mimi nina imani ya kwamba ikiwa Tume hii itapewa nafasi ya kuhudumu kulingana na misingi ya sheria hii tunayojadili wakati huu na vile vile misingi ya Katiba, basi tutaweza kupata majibu kwa baadhi ya maswala haya nyeti yaliyo na uzito mkubwa. Mimi vile vile ingawa ninajua kwamba kuna Mswada wa kando kuhusu Tume ya Jinsia na Usawa, ningependa kusema ninaunga hatua hiyo ya kutenga tume hizi mbili ili tuweze kuwa na tume hii ya kushughulikia maswala ya haki na vile vile tume tofauti itakayoshughulikia maswala ya jinsia na usawa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninamshukuru Waziri wa Haki tena. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono."
}