GET /api/v0.1/hansard/entries/33197/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33197,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33197/?format=api",
    "text_counter": 443,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Mswada huu umewasilishwa wakati unaofaa. Mswada huu unahusu kutekelezwa kwa Katiba yetu. Huu ni mojawapo wa Miswada tunaohitajika kupitisha. wananchi wanataka tupitishe Miswada hii kwa haraka sana ili waweze kufurahia matunda ya Katiba mpya. Jambo la pili ni kuwa Mswada huu unazingatia haki za maisha ya binadamu katika nchi yetu. Ikiwa tutaupitisha Mswada huu, basi mambo haya yatekelezwe mara moja. Mswada huu hautakuwa na maana kwa wananchi ikiwa tutakuwa na vikundi vitatu vya watu; wale watatii sheria, wengine watakuwa wakitaka kutii sheria kwa mbali na wengine watapenda kuvunja sheria hii wakiwa usukani au mamlakani. Kwa nini ninasema hivyo? Hii ni kwa sababu miaka mingi tulikaliwa na mkoloni aliyevunja haki za binadamu za Mwaafrika. Tuliupigania Uhuru wetu na tulipopata Uhuru, tulishangilia utawala wa Mwafrika na tukasema tutaheshimu haki zetu. Ni dhahiri kuwa mambo yote yalienda kinyume na matarajio yetu. Tumeshuhudia vifo vya watu vya watu mashuhuri na wa kawaida katika nchi yetu tukufu hapa. Mauaji haya yalitekelezwa na watu fulani. Hata hivyo, wale waliohusika na mauaji haya hawajawahi kufikishwa mahakamani. Sheria za nchi hii huumiza sana watu wanyonge. Ikiwa mtu ataiba kuku, anachukuliwa hatua kali sana. Wakati mwingi, mwizi wa kuku hufungwa zaidi ya miaka 10. Lakini wanaoua wenzao na kupora mali ya wananchi wa Kenya kwa sababu wako madarakani, wanaachiliwa huru. Ikiwa Tume hii haitatekeleza kazi yake inavyotakikana, basi tutakuwa tunapoteza wakati wetu hapa Bungeni."
}