GET /api/v0.1/hansard/entries/33200/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 33200,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33200/?format=api",
"text_counter": 446,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Watu wengi wametezwe katika nchi hii. Mwaka wa 1992, tulishuhudia mateso makubwa ya baadhi ya Wakenya. Wana haki sawa na watu wengine katika nchi hiii. Hata hivyo, walipigwa na kuhamishwa kutoka makao yao. Mpaka leo, hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikishwa kortini kujibu mashtaka kuhusiana na mateso na maafa yaliyowakumba watu hawa mwaka wa 1992. Ni aibu iliyoje kuona sisi tunaendelea kupokea mishahara yetu ili watu wetu wanaendelea kuteseka hemani? Wakati wa uchaguzi wa mwaka 1997, tulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na watu wengi walitimuliwa kutoka makao yao. Watu hawa hakuwa na hatia yoyote ila tu kupiga kura zao. Sasa watu hawa wanaishi maisha ya umaskini sana. Mali yao yaliharibiwa. Ni aibu iliyoje baada ya vita hivi, Serikali huunda tume ya kuchunguza chanzo cha vita hivi? Pesa nyingi hutumika lakini hakuna funzo tunalopata. Ripoti huandikwa lakini hakuna yeyote ambaye yuko tayari kutekeleza mapendekezo ambayo yanatolewa na tume hizo. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2002, hali haikuwa tofauti. Watu walitimuliwa kutoka mashamba yao na mali mengi yakaharibiwa. Kilele cha vita hivi kilikuwa mwaka wa 2007. Watu wengi walipoteza maisha yao na mali yao yaliharibiwa. Leo hii wanaishi ndani ya hema wakiwa na watoto wao. Hii ni aibu kubwa kwa nchi hii. Zaidi ya watu 3,000 na watoto wao waishi hemani. Inahitajika tujiulize ni kwa nini mambo haya hutokea wakati wa uchaguzi. Je, ni viongozi ambao huchochea watu kupigana? Ikiwa viongozi, wananchi wanaweza kuzingatia maneno ya uzalendo yaliyo katika wimbo wetu wa taifa, basi “tutaishi kwa amani”. Tunataka kuona Tume itakayozingatia haki na umoja wa wananchi wote. Kwa hivyo, tunataka Mswada huu upitishwe mara moja ili tuunde Tume hii itayojishughulisha na haki za binadamu. Ninakumbuka zaidi ya miaka 48 nilipokuwa kijana mdogo niliona ndege za kutoka Marekani zikiwa zimebeba mahindi na kuleta katika eneo langu la Bunge. Huu ulikuwa ni wakati wa Rais J.F. Kennedy. Hii ilikuwa ni baada ya nchi yetu kupata Uhuru. Nimeishi kwa heshima na kuendeleza uzalendo wangu bila chuki. Mimi ni mzee wa miaka 58. Miaka hii yote sijawahi kuona nchi hii ikiwa na chakula cha kutosha. Serikali ambayo haiwezi kuwalisha wananchi wake haistahili kuongoza. Wakati huu tunajenga barabara za gorofa lakini tumeshindwa kuwalisha wananchi wetu. Ni fedheha ilioyoje kuona katika runinga zetu watu ambao wamekonda sana hadi mbavu zao zinaonekana? Wengine wamepoteza nywele zao kwa sababu ya njaa. Je, ni haki kwa Mawaziri na Wabunge kuendesha magari makubwa ilhali watu wetu wanaendelea kufa njaa? Taifa huru linaunda tume ya haki za binadamu lakini tayari tunavunja sheria huku tukijuvuna kwamba kijikaratasi kitaweza kubadilisha maisha yetu. Wakenya wanafaa kuamka na kujua kwamba sisi ni viongozi ambao tunataka kuongoza watu kwenye ahadi ya usawa ili waweze kuishi."
}