GET /api/v0.1/hansard/entries/33207/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 33207,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33207/?format=api",
"text_counter": 453,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Juzi, tumeona wakulima wa Bonde la Ufa wakiwa na magunia ya mahindi. Inasemekana kwamba gunia moja linauzwa kwa Kshs2,500. Utawala wa nchi hii kutoka juu unakaa chini ya kinara ambaye in mwenyekiti wa ulinzi wa chakula katika taifa letu na wanaamua kutoa mahindi katika Afrika Kusini kwa Kshs3,600 huku tunanyamazishwa ilhali kuna sheria ya kulinda jambo hilo. Tunaambiwa kwamba hiki kijikaratasi kitaweza kulinda haki ya binadamu. Bw. Naibu Spika wa Muda, moyo wangu unalia kila siku. Haifai kuwa tunakaa katika nchi na kutumia fedha namna hii huku tukifanya mambo ya kujionyesha tu lakini hatuitii sheria. Tutapitisha Mswada huu. Si kazi ya Waziri kuona kwamba kila mtu anatii sheria, lakini ni sisi viongozi kuona kwamba tunaitumia haki. Kutakuwa na unyanyasaji gani kuliko kuona kwamba unaamka asubuhi na kusoma historia ya wizi na kamba, rasilmali imeibiwa na yule mtu ambaye ni mlinzi wa haki hiyo? Sisi tunaamka na tunakuja hapa Bungeni, tunasalimiana kwa mikono na tunacheka huku waliotuchagua wakijua kwamba tumewadhulumu kwa kuyafanya mambo hayo."
}