GET /api/v0.1/hansard/entries/33208/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33208,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33208/?format=api",
    "text_counter": 454,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Watoto wa miaka mitatu au minne wananajiswa. Huu ni unajisi wa hali ya juu. Tunasoma kwenye magazeti kwamba mtoto amenajisiwa na aliyefanya kitendo hicho ni mtu mzima anapelekwa kortini na anapewa bondi na anaenda nyumbani. Mtoto huyu amedhulumiwa na hataweza kusahau kilichotokea katika maisha yake. Aliyemfanyia mambo hayo anaenda nyumbani na kuwakemea wazazi wa mtoto huyo. Hii inakuwa ni shida mara mbili. Mwenye kuumizwa na mwenye kumlea, wote wako taabani. Ninaomba tupitishe Mswada huu lakini tuweke akili zetu sawa sawa kwa kutii sheria na kufahamu kwamba yale ambayo ile sheria tunayovunja hapa, wananchi wa Kenya wanaona."
}