GET /api/v0.1/hansard/entries/33211/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33211,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33211/?format=api",
    "text_counter": 457,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Baiya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 8,
        "legal_name": "Peter Njoroge Baiya",
        "slug": "peter-baiya"
    },
    "content": "Tuko na Kamati ya Haki za Binadamu na pia juzi, tulipata yale matarajio ambayo tunaweza kutarajia kutokana na utekelezaji wa sheria hii. Ninaunga mkono maoni ambayo yametolewa na waliozungumza mbele yangu kwamba katika nchi hii, tangu zamani, Katiba ya nchi hii imekuwa na sura ya kupeana haki kwa binadamu. Lakini ukweli ni kwamba, katika historia yetu kama taifa, kuanzia wakati wa Ukoloni, tumekuwa na tabia na mazoea mabaya. Wanaotakiwa kuiga sheria na kutoa huduma kwa nchi hii hawaheshimu haki za binadamu. Hii tabia mbaya na mazoea mabaya yalianza wakati wa ukoloni, hasa, katika harakati za kukomboa nchi hii ambapo vikosi vya usalama vilitumika kukandamiza wananchi na kuwapeleka mahakamani bila kujali haki zao. Hata wakawa wanafanyiwa kesi mahakamani bila kujali haki zao. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati tulipata Uhuru, wengine walipoteza haki na pia ari yao. Wengi waliuwawa kinyama na wakati tulipopata Uhuru, matarajio ya wananchi yalikuwa kwamba uhuru uliwatoa kwenye dhuluma za wakati wa ukoloni. La kushangaza ni kwamba, hata wakati tulipata Uhuru, badala ya kurekebisha na kubadilisha mwelekeo wa Serikali ya Ukoloni, tuliendelea na ile tabia. Hii Kamati ya Haki za Binadamu iliundwa juzi na tunajua vile ambavyo imekuwa ikifanya kazi. Wakati mwingine, imepata pingamizi kubwa kutoka kwa Serikali ilhali"
}