GET /api/v0.1/hansard/entries/33214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33214/?format=api",
    "text_counter": 460,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wao ndio wanafaa kuheshimu na kutekeleza sheria na kuhakikisha kwamba wameheshimu haki za binadamu za wakenya wote. Shida hii inaanzia kwa viongozi wa idara mbalimbali. Tunataka huu Mswada uwe kielelezo ama chanzo cha kuhakisha kwamba kila mtu anawajibika kuhakikisha kwamba amefanya kazi vilivyo. Inafaa Kamati ya Haki za Binadamu ihakikishie taifa kwamba Serikali inaheshimu haki za binadamu. Ni wazi kwamba hatuwezi kuhakikishia wananchi kwamba tunaheshimu haki zao za kibinadamu kama hatujahakikisha kwamba mazingira ya kuendeleza shughuli hizo inaheshimu haki za kibinadamu. Kama hatujapigana na umaskini, ukosefu wa nafasi za kazi kwa wananchi na kuwepo kwa sera ambazo zitahakikisha kwamba nchi hii inaendeleza shughuli za kutoa hudumu zifaazo kwa wananchi, tutakuwa tunawandanganya wananchi kuwa tutawahakikishia haki zao kama Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama taifa, tusipojaribu kupambana na umaskini na ukosefu wa nafasi za kazi, na kuweka sera ambazo zitahakikisha kwamba nchi hii inaendeleza shughuli za kutoa huduma zinazofaa kwa wananchi, tutakuwa tunawadanganya wananchi kwamba tutawahakikishia haki zao kama Wakenya. Kuna shida shida nyingine, kama zilivyoangaziwa, ambazo pia zinachangia kukandamizwa kwa haki za kibinadamu. Shida hizo ni kama ufisadi, wizi wa mali ya umma, na nyinginezo. Tunaposhughulikia haki za kibinadamu, kulingana na Katiba, matarajio yetu ni kwamba Serikali itahakikisha kwamba tunasawazisha mazingira ili tuwezeshe shughuli za Serikali sio tu kwenye Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu bali pia tuweze kuheshimu haki za kibanadamu katika mpangilio wa shughuli za Serikali kwa jumla. Hii inatuelekeza kufikiria juu ya Tume nyingine kama Tume ya Kupambana na Ufisadi Nchini, na ile sheria inayowataka maafisa wa umma kuwajibika vilivyo na kuhakikisha kwamba wametoa huduma vilivyo kwa wananchi, na kwamba wasipofanya hivyo Serikali itawachukulia hatua kabambe, kulingana na sheria iliyopo na Katiba, ili tuweze kuwahakikishia Wakenya kwamba, kama taifa, tuna mwelekeo mpya – mwelekeo unaowaheshimu Wakenya kwa jumla ili waweze kuvuna matunda ya haki zao za kibinadamu. Pia, tunaihimiza Serikali iitengee Tume hii pesa za kutosha ili iweze kutekeleza shughuli zake. Hatungependa Serikali ifanye kama vile tulivyoona ikifanya zamani. Kwa mfano, katika miaka iliyopita, iwapo Serikali haikufurahishwa na shughuli za Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, ilikuwa ikiinyima pesa Tume hiyo ili kuipunguzia uwezo wa kufanya kazi yake. Bw. Naibu Spika wa Muda, kumekuwa na shida ya Serikali kukosa kukabiliana na matatizo fulani. Kumekuwa na ukiukaji wa haki za kikatiba. Kwa mfano, tumekuwa na tabia ya kuwatenga vijana kwa sababu wao ni vijana, na hata kuwawekelea majina mabaya kama vile Mungiki na mengine, kikiwa kielelezo cha kuwakandamiza, na kuwasingizia kwamba eti hawatii sheria. Huu ni ukiukaji wa sheria kwa sababu haki ya kwanza ya mwananchi ni kutodhulumiwa ama kutochukuliwa hatua bila kufuata mpangilio wa sheria. Kwa hivyo, huu ni Mswada muhimu ambao utaisadia nchi hii kuhakikisha kwamba tumeweka msingi unaofaa kuhakisha kwamba haki za kibinadamu zinalindwa na sheria. Hata hivyo, inafaa ifahamike kwamba hii sheria, ikiwa peke yake, haiwezi kuwahakikishia Wakenya haki zao za kibinadamu. Hilo linawezekana tu tukihakisha kwamba tumetekeleza mabadiliko na kuchukua mwelekeo mpya, kama inavyotarajiwa kwenye Katiba mpya. Tunatakiwa kuchukua mwelekeo mpya na kuwahakikishia"
}