GET /api/v0.1/hansard/entries/33338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 33338,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/33338/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Otuoma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 132,
        "legal_name": "Paul Nyongesa Otuoma",
        "slug": "paul-otuoma"
    },
    "content": "Bw. Spika, tulianza na Kshs50,000 ambayo ilikuwa ikipewa kila kikundi. Kuanzia mwaka huu, tuliongezea fedha hizo kulingana na mahitaji ya vikundi hivyo. Sasa wanaweza kuchukua Kshs50,000, Kshs100,000 au Kshs500,000 kulingana na vile watakavyokuwa wametimiza yale matarajio ambayo yamewekwa. Lakini pia tunakubali kuwa wakati huu mpango wa fedha kwa vijana ulipoanzishwa, kulikuwa na fedha ambazo zilitoka kwa Serikali na ikawa kuwa mashirika ya biashara yatafanya kazi nasi ili kuongezea zile fedha na kupitia benki na mashirika ya fedha, kuna vikundi ambavyo vimepata hata zaidi ya Kshs1 milioni kulingana na vile walivyoweza kuyatimiza matarajio ya kukopa."
}