GET /api/v0.1/hansard/entries/333748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 333748,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/333748/?format=api",
"text_counter": 256,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika Muda, nakubaliana na Wabunge wenzangu kwamba wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Wametoa ulalamishi hapa. Nimejaribu kuchangia na kusaidia Mawaziri kuja lakini kama Kiranja wa Serikali mwenyewe anauliza taarifa na inachukua majumaa manne na bado haijatolewa na hili ni jambo muhimu sana ambalo linahusu taifa nzima, hivyo si vizuri. Bw. Naibu Spika, kama kule umezaliwa kuna watu wengi sana ambao wanataka kuwa viongozi, ukiangalia mazingira yaliotolewa na Serikali kutoa kiwango cha elimu katika sehemu hiyo, huwezi kulinganisha na sehemu zingine. Kule kuna watu ambao wamezaliwa kama viongozi na kwa sasa wanafungiwa. Korti ambayo Waziri mwenyewe anasimamia imetoa uamuzi na kusema kwamba kipengele fulani na fulani kimetolewa na huyu Waziri ambaye analinda na kusimamia sheria anaweza kuamuru Tume ambayo anasimamia kuwaambia kwamba yale mambo mnatangaza na kudhani kwamba yanatakiwa katika kiwango cha wananchi kusimama sio halali. Waziri wa sheria anasimamia uongo na udanganyifu kwa sababu kama hatoi taarifa kule mashinani kuwaambia watu wake, basi kuna mwongo gani kuliko huyo? Bw. Naibu Spika, ninataka utoe uamuzi kama Waziri huoy kweli anastahili kufanya mambo kama hayo na kuzua kasheshe na taharuki katika nchi nzima."
}