GET /api/v0.1/hansard/entries/334071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 334071,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/334071/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama kuunga mkono na kumpongeza Waziri Sally Kosgei kwa kuleta Mswada huu hapa ili tuujadili. Wakulima nchini Kenya wamekuwa na matatizo mengi sana. Kwa sababu ya matatizo ambayo wamekuwa nayo, hawakufanya kazi na kupata mavuno kulingana na nguvu walizozitumia. Ninataka kuzungumzia sana swala la halmashauri ambayo Waziri atabuni ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanapata lishe bora and vile vile uongezaji wa thamani ya mavuno ambayo wakulima wamekuwa wakipata. Pia, kuna swala la unyunyizaji maji mashambani. Jukumu hili limepatiwa Wizara ya Maji, lakini lilikuwa nzito na linatakiwa kuangaliwa kwa undani ili wale wakulima wenye kunyunyizia mashamba yao maji waweze kufanya kazi na Serikali ili kuhakikishia kuwa maji haya yameweza kufika na kuwawezesha kupata kiwango cha chakula cha kuwawezesha kupata lishe bora. Vile vile, maeneo kama ya kwetu - upande wa Taveta - ambapo wakulima wetu wanakuza ndizi kwa wingi, vitunguu na nyanya, wamekuwa wakiteseka sana kwa sababu hawana vyeti vya kumiliki ardhi. Kwa hivyo, hawawezi kupata mikopo inayostahili. Bw. Naibu Spika wa Muda, nimefurahi kuwa kumetajwa hazina ya kuweza kuwasaidia wakulima wapate pesa za kuweza kununua mbolea za kuwasaidia kuweza kupata chakula na mavuno kwa wingi. Hii ni kwa sababu watu wetu wengi ni wale wenye mashamba madogo madogo. Hazina hii itaweza kuwasaidia wakulima nchini kote. Ni hazina ambayo ninatumai wakulima wote nchini wamekuwa wakiingojea ili waweze kufanya kazi zao bila wasiwasi. Hazina hii itawawezesha kupata pesa za kutosha ili waweze kupata mavuno vilivyo. Uuzaji wa mavuno nchini na nje ya nchi ni kitu ambacho kimetatiza watu wengi sana kwa sababu maeneo yetu yana barabara mbovu. Kwa hivyo inabidi wakulima katika maeneo haya kutumia pesa nyingi ili waweze kupeleka mavuno yao sokoni. Mara nyingi, mavuno mengine yanaharibikia njiani kwa sababu ya shida za uchukuzi. Ninatumai kwamba bima ya mimea na mavuno itakuwa muhimu sana kwa sababu itawasaidia wakulima ambao wamepata hasara haswa wakati wa ukame na mafuriko. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, ningependekeza kuwa dada yangu, Dkt. Sally, aweke mstari wa mbele swala la kuandikisha wafanyakazi wa kutosha ili wakulima waweze kupewa masomo ya kutosha ili wafanye kilimo cha kisasa na sio cha zamani. Kule mashambani mara nyingi wale wakulima wamezoea kulima kulingana na mila na desturi zetu. Lakini wakipatiwa wafanyakazi ambao wamefunzwa ukulima wa kisasa, watafundishwa. Lakini hatuwezi kuwa na wafanyakazi hawa kama vyuo vikuu haviwezi kusomesha watu wa kutosha katika maswala ya ukulima. Kama hawataweza kuwasomesha wanafunzi wengi ili waweze kwenda hadi mashinani kuwafunza wakulima jinsi ya kufanya kazi, basi yote haya tunayoyafanya yataishia patupu. Hii ni kama hatutaweza kupata wafanyakazi wa kutosha."
}