GET /api/v0.1/hansard/entries/335096/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 335096,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/335096/?format=api",
"text_counter": 491,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "The Minister for Youth Affairs and Sports",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": " Bi Naibu Spika wa Muda, kwanza nataka kumshukuru Mhe. Sophia Noor kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Pia ninamshukuru kwa kunipa dakika moja ili nitoa machango wangu juu ya Mswada huu. Kwanza ningependa kutoa hongera zangu kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali (NGOs) kwa mchango wao was maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini. Hii ni dhihirisho kuwa Wakenya wakipewa nafasi katika viwango mbalimbali watachangia maendeleo ya nchi hii vilivyo. Ningependa kusisitiza swala la uajibikaji katika mashirika haya. Kila mara Wakenya na mashirika haya yanataka kuona Serikali ikiajibika katika matumizi yake ya pesa za umma. Hili ni wazo nzuri kwa sababu tukizitumia pesa zetu vizuri tutakuwa na maendeleo mengi hapa nchini. Vile vile tungependa kuona mashirika haya yakiajibika katika matumizi ya pesa wanazopata kutoka nje ya nchi kuambatana na mwamko mpya wa nchi hii. Kwa hivyo, tunengependa wote tuajibike kama Serikali na kama mashirika haya yasiyo ya kiserikali. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}