GET /api/v0.1/hansard/entries/3357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 3357,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/3357/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, watu waliosajiliwa kwa ujumla katika wilaya ya Bura walikuwa 854, lakini kwa kutegemea pesa tulizopata, watu 600 pekee ndio wamekuwa wakilipwa. Hawa watu 150 kutoka Madogo wataendelea kulipwa, ijapokuwa kumekuwa na kucheleweshwa kwa malipo kwa sababu ya shughuli za kuwasajili kupitia kwa mpango na mtandao uliyoko katika posta. Vile vile, watu 213 katika kata ya Bura wamekuwa wakilipwa, na mwezi huu wa Disemba hautaisha kabla hawajalipwa. Nataka kuwahakikishia watu wote wa Bura, ambao wamekuwa wakipata pesa hizo katika mradi huu, kwamba pesa zao zipo na wataendelea kupata haki yao bila shida. Tatizo lilitokea kuchelewesha malipo kwa sababu ya usajili na posta. Asante sana."
}