GET /api/v0.1/hansard/entries/341732/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 341732,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/341732/?format=api",
"text_counter": 497,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Minister for Fisheries Development",
"speaker": {
"id": 27,
"legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
"slug": "amason-kingi"
},
"content": " Bw. Spika, asante kwa kunipatia fursa hii angalau pia na mimi nitoe shukrani zangu. Kwa niamba yangu binafsi na kwa niamba ya watu walionileta hapa Bunge, watu wa Magarini, ningependa kupeana shukrani zangu kwa Rais wetu kwa kazi njema aliyoifanya. Ikiwa kuna kitu ambacho nimejifunza kama kijana kutoka kwa Mzee wetu Rais wetu, ni nguvu ya maneno machache ama nguvu ya kimwa. The power of silence. Mhe. Rais ni mchache sana kwa maneno. Lakini kama tujuavyo, mtu yeyote ambaye ni mchapakazi hatumii kinywa chake wakati mwingi. Na kwa sababu ya yale aliyotufanyia, kusema kweli kama Wakenya na Wabunge wa Bunge hili la Kumi, tunaweza kuweka kifua mbele na kumwambia Mhe. Rais asante na kumwombea, akielekea kule kustaafu, Mwenyezi Mungu ampatie maisha marefu yasiyokuwa na bughudha. Asante sana, Mhe. Rais."
}