GET /api/v0.1/hansard/entries/341738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 341738,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/341738/?format=api",
    "text_counter": 503,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, nakushukuru kwa nafasi hii nami niweze kuungana na wenzangu kumshukuru Rais kwa mambo mengi ambayo amefanyia taifa hili. Mwishowe nataka kutaja mambo mawili ambayo Wakenya hawatasahau katika maisha yao. Jambo la kwanza ni kwamba Rais ametoa elimu ya bure kwa watoto wa maskini ambao kila siku kila mzazi anamuombea Rais kwa kuona kwamba mtoto wake anasoma bila taabu. Jambo la pili, namshukuru Rais kwa sababu amewaondolea wazazi maskini mzigo wa kuitishwa pesa ya harambee ya kujenga shule. Kwa hivyo, ametoa elimu ya bure na vile vile pesa ya kujenga shule ili watoto wasome bila kuhangaika. Kwa hivyo, ningependa kutoa shukrani zangu na hivi leo unapoanza kuondoka ukumbuke ya kwamba Wakenya wote na haswa maskini ambao Mungu anasikia maombi yao wanakuombea siku nenda, siku rudi. Kwa hivyo, Mungu akujalie na akuongezee nguvu zaidi za kuweza kutumikia taifa na vile vile kuwasaidia katika uongozi kwani uongozi wako hauna masengenyo, chuki na tumekaa hapa tukifanya kazi yetu bila kutushurutisha na maneno ya kutishia."
}