GET /api/v0.1/hansard/entries/345230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 345230,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/345230/?format=api",
"text_counter": 627,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Munya",
"speaker_title": "The Assistant Minister for East African Community",
"speaker": {
"id": 279,
"legal_name": "Joseph Konzolo Munyao",
"slug": "joseph-munyao"
},
"content": " Bi. Naibu Spika wa Muda, mimi pia nataka kuunga Mswada huu mkono kwa dhati. Afisi ya chifu ni muhimu sana katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali mashinani. Katiba ya Kenya ambayo ilipitishwa na wananchi wa Kenya haikupiga marufuku ofisi ya chifu. Ilisema marekebisho yafanywe katika ofisi ya chifu na ya mkuu wa wilaya ili zifanye kazi sambamba na serikali ya kaunti. Kwa hivyo, Mswada huu unaidhinisha msimamo wa Katiba ya Kenya juu ya ofisi hizi. Machifu na wenzao wanaofanya kazi katika Serikali ya Wilaya wasiwe na wasiwasi wowote. Kazi yao imejikita katika Katiba ya nchi hii. Wataendelea kutekeleza majukumu yao na kupata mishahara na marupurupu mengine. Huduma zao ni muhimu kwa wananchi wote. Ofisi hizi ni nguzo muhimu katika utawala wa nchi hii. Lakini ya muhimu ni kwamba maafisa wa kaunti watakaokuwa wakifanyia wananchi kazi uko mashinani watafanya pamoja na machifu na viongozi wengine wa kimkoa. Hakutakuwa na vita baina yao. La muhimu kwetu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma. Sisi sote tukifanya kazi pamoja, tutaweza kuwahudumia wananchi wote."
}