GET /api/v0.1/hansard/entries/345270/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 345270,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/345270/?format=api",
"text_counter": 667,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Godhana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 23,
"legal_name": "Dhadho Gaddae Godhana",
"slug": "dhadho-godhana"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo ninataka kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Waziri. Kinyume na tetesi, hofu, uvumi na propaganda ambazo zilikuwepo hapo mbeleni kwamba itakapopitishwa kazi za machifu zitakuwa hazina maana kamwe na watafutwa waende nyumbani. Mswada huu umethibitisha wazi kwamba hiyo ilikuwa siasa na propaganda na wala haikuwa ukweli. Mswada huu unathibitisha mawazo ambayo Serikali pamoja na viongozi wamekuwa wakitoa kwamba kamwe machifu hawatafutwa kazi. Mswada huu unaonyesha wazi kuwa kazi ya machifu, naibu wao na hata wazee wa vijiji imetambulika na wanasiasa wote na Bunge hili. Kazi hii imepitishwa rasmi kupitia Mswada huu na tunasema kazi yao iendelee. Naibu Spika wa Muda, ingawaje tunapitisha Mswada huu, ningetaka kumwambia Waziri kwamba tungependelea maisha ya machifu na naibu wao yaangaliwe siku sijazo ili waweze kutenda kazi wakiwa na motisha zaidi. Hii ni kama vile kupewa marupurupu ya nyumba. Tungetaka kuwaona machifu wakiwa na mikakati ya kuwawezeshe kununua magari. Wapewe risk allowances ambazo zitawatia motisha zaidi ili waweze kufanya kazi kwa urahisi na kufurahia maisha yao ya kazi ya uchifu. Kusema ukweli, sisi ambao tunawajua machifu na tumefanya kazi nao, ingawaje wanafanya kazi kwa kujitolea, kuna mambo mengi ambayo yanahitajika ili kuwatia motisha ili waweze kutenda kazi yao kwa bidii zaidi. Kwa hayo machache, ningependa kuunga mkono na kumpongeza Waziri kwa sababu ya Mswada huu."
}