GET /api/v0.1/hansard/entries/345299/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 345299,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/345299/?format=api",
"text_counter": 696,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kamama",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Higher Education, Science and Technology",
"speaker": {
"id": 165,
"legal_name": "Asman Abongutum Kamama",
"slug": "asman-kamama"
},
"content": " Bi Naibu Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kuunga mkono Mswada huu wa utawala wa mikoa. Tunahitaji utawala wa mikoa ili tuweze kuhakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha mashinani. Vile vile, tunahitaji utawala kama huu kwa sababu majirani wetu, kwa mfano, huko Uganda wana watu wanaoitwa ResidentCommissioners. Kuna watu kama hawa wa utawala katika Zimbabwe. Ufaransa kuna utaratibu ambao unaitwa prefecture. Kwa hivyo, ni vizuri sisi kama viongozi wa nchi hii kuunga mkono huu Mswada. Sisi sote tunajua kwamba machifu wanafanya kazi nzuri kuhakikisha kwamba kuna usalama katika vijiji vyote nchini. Wanafanya kazi ambazo polisi wa kawaida hawawezi kufanya. Kuna mizozo ambayo hutokea mashinani ambayo hutatuliwa na machifu na manaibu wao. Kwa vile Waziri yuko hapa na kwa sababu mimi pia zamani nilifanya kazi katika utawala wa mikoa, ningependa kutaja vifaa vinavyohitajika. Kwa mfano, machifu wanahitaji pikipiki. Mimi mwenyewe, kupitia CDF, nilipatiana pikipiki kumi katika eneo langu. Ikiwa inawezekana, ningependa kila chifu na mdogo wa kata wapatiwe pikipiki ili waweze kutekeleza kazi yao inavyotakikana. Kwa hayo machache, naunga mkono kwa nguvu zote."
}