GET /api/v0.1/hansard/entries/346635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 346635,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/346635/?format=api",
    "text_counter": 592,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Maj-Gen. Nkaisserry",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Defence",
    "speaker": {
        "id": 192,
        "legal_name": "Joseph Kasaine Ole Nkaissery",
        "slug": "joseph-nkaissery"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa muda huu ili niweze kuunga mkono Mswada huu. Tangu mimi niwe Mbunge miaka kumi iliyopita, sijawahi kuongea kwa Kiswahili. Kwa hivyo, ningependa kufanya historia kwa kuzungumza katika lugha hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu machifu wako na kazi muhimu sana nchini Kenya. Kazi hiyo ni kazi ya usalama. Serikali kuanzia kwa Rais mpaka chini kwa county commissioner, ward coordinator, chifu na naibu wa chifu ni sehemu moja ambayo ina maana sana kwa nchi yetu. Mswada huu unasema kwamba Serikali ya kaunti haisikii kamwe usalama wa nchi. Ni Serikali kuu ambayo inahusika. Hapo ndipo tumeleta Mswada huu ili tupate nguzo kamili kiusalama nchini."
}