GET /api/v0.1/hansard/entries/346639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 346639,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/346639/?format=api",
"text_counter": 596,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mrs. Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuunga mkono Mswada huu. Ningependa kuungana na wenzangu ili kuchangia mambo ya machifu. Vile machifu na manaibu wao wanafanya kazi katika kata ndogo na tarafa, inaonekana hawa ni watu ambao wako tayari kufanyia nchi yetu kazi bila kubagua mtu na bila kuingia siasa. Hawa ni watu wemejitolea kwa kila njia ili kufanya kazi kwa nchi yetu bila kubagua mtu yeyote. Hawa ni watu ambao wanafanya kazi nyingi. Ukiangalia kazi ya chifu utapata kwamba anafanya kazi kama ya koti. Utapata kwamba watu wanapeleka kesi kwake kabla ifikishwe kwa Mkuu wa Wilaya. Utapata kwamba katika mambo ya usalama ni wao ambao wanakimbia hapa na pale kuleta ripoti haswa sehemu ambazo kuna mizozo. Kwa hivyo, hawa ni watu ambao wamejitolea. Hakuna haja ya kusema kwamba hawana kazi. Hawa wote ni watu ambao wanashirikiana na wananchi ili kufanya kazi inavyotakikana. Hapa kwa machifu na manaibu wao ndio kuna nafasi ambao pia akina mama wanaweza kupata kazi. Hapo mbeleni haingewezekana akina mama kuwa machifu ama hata manaibu. Sasa akina mama pia wanajivunia kuwa machifu ama manaibu wa machifu. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}