GET /api/v0.1/hansard/entries/34819/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 34819,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/34819/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Nuh",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 114,
"legal_name": "Nuh Nassir Abdi",
"slug": "nuh-abdi"
},
"content": "Nashukuru, Bw. Spika. Katika Ripoti ya WHO aliyoisoma Bw. Waziri Mkuu, katika sentensi mbili za mwisho, alisema kwamba matumizi ya vyakula vya GMO kwa muda mrefu na utafiti katika soko utachangia kujua usalama wake katika maswala ya kiafya. Ningependa kujua ikiwa Waziri Mkuu anaweza kukiri kwamba utafiti unaotumika sasa hivi kujua kwamba chakula cha GMO kiko salama kiafya, ni utafiti uliotokana na chakula hicho kulishwa panya kwa muda wa miezi mitatu? Utafiti ambao ungeweza kubaini madhara ya kutumia vyakula vya GMO kutoka kwa matumizi ya mwaka moja, miaka 10 ama miaka 12 – ambayo inaleta hofu ya magonjwa kama saratani na mengine – mpaka wa leo bado haujabuniwa."
}