GET /api/v0.1/hansard/entries/349177/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 349177,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/349177/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "waliopoteza wapendwa wao jana kule Garsen. Ninataka niwashauri, niwasihi na niwaombe kwamba wawe watulivu, na wasiendelee kupigana. Ninawasihi wasitishe mapigano hayo kwa sababu hatua ambayo Serikali imechukua, ya kujaribu kutuliza mtafaruku huo ni muhimu sana. Ninaipongeza hatu ya Serikali ya kubuni tume ya kuuchunguza mtafaruku huo ili kubainisha sababu za matukio hayo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuleta uwiano na hali ya amani katika kaunti ya Tana River. Kuendelea kupigana kunaweza kutatiza hali ambayo sisi sote, kama Wakenya na wakazi wa kaunti yaTana, tungependa kuiafikia. Kwa hivyo, kama kiongozi wa sehemu hiyo, ningependa kuwasihi sana wakazi wa Tana River kwamba tuchukue mwelekeo huo. Nimeshaongea na Waziri na tumekubaliana na hata Serikali imechukua msimamo huo. Tungependa tume iliyotumwa kule iharakishe mipango ya kukamilisha Ripoti yake. Pia tunataka uchunguzi unaofanywa na maafisa wa vitengo vya Criminal Investigations Department (CID) na National Intelligence Service (NIS) uharakishwe ili hatua mwafaka za kisheria ziweze kuchukuliwa. Juhudi hizo zote zinalenga kupelekea kuweko kwa amani katika sehemu hiyo. Kwa hivyo, ninawaomba wakazi wa sehemu hiyo wawe watulivu tungojee hatua ambazo Serikali itachukua baada ya Ripoti ya Tume hiyo kutolewa. Bw. Naibu Spika wa Muda, sasa ninataka kuipongeza Serikali ya Muungano. Kuseme kweli tumetoka mbali. Kufikia siku hii ya leo, tumepiga hatua kubwa. Haikuwa rahisi. Kulikuwa na mivutano hapa na pale; mivutano ambayo wakati mwingine ilituweka katika hali ya taharuki. Hata hivyo, mivutano hiyo ilikuwa muhimu kwa sababu imetuwezesha kufika mahali tulipo hivi sasa. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuongoza mpaka tukafika mahali tulipo hivi sasa. Hata hivyo, haingekuwa rahisi kwetu sisi kufika tulipo sasa bila ya Bunge hili na Spika kusimama kidete na kutoa uongozi mwafaka. Spika amefanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa na kuweza kupata pongezi kutoka kwa watu wengi, wakiwemo Wakenya. Watu kwote ulimwenguni wametambua kazi aliyofanya katika Bunge hili. Amekuwa akichukua msimamo wa kutoegemea upande wowote wakati wa mvutano miongoni mwa mibabe Serikalini. Hii ilikuwa ni kazi ngumu, lakini aliifanya kwa njia ya hekima na busara nyingi. Ni lazima tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpatia hekima kama hiyo na kuweza kutufikisha mahali tulipo sasa. Ninawapongeza Wabunge wote waliokuwa katika Bunge hili na kuweza kufanya yale yote waliyofanya. Wamefanya kazi ngumu. Kazi hiyo haikuwa rahisi, na haswa kutekeleza ahadi walizotoa kule mashinani walipokuwa wakiwania viti vya Bunge na vile vile kutekeleza shughuli hapa Bungeni na kutekeleza wajibu wao nyumbani kwao. Ninajua kwamba walijitolea sana, wakajinyima na kunyima jamii zao kwa sababu ya kutekelezea kazi Wakenya. Ninawaombea kwamba wanaporudi mashinani kutafuta kura waweze kuangaliwa na wananchi ili kile watakachoomba wapatiwe. Pia ningependa kupongeza Kenya Defence Forces (KDF). Watu wengi hajaelewa jinsi kazi hiyo ilivyotekelezwa. Haikuwa kazi rahisi. Kazi ya kuleta amani nchini Somalia haikuwa rahisi. Ilikuwa kazi ngumu lakini KDF waliifanya kwa uadilifu, na wanastahili pongezi. Ninajua kwamba sasa, kinyume na dhana za hapo awali---"
}