GET /api/v0.1/hansard/entries/349209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 349209,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/349209/?format=api",
    "text_counter": 315,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "la Kumi na kuweza kuwasaidia na kuwahudumia Wakenya wote kwa jumla. Pia nachukua nafasi hii kuwashukuru Wabunge wenzangu wote ambao tulishirikiana uzuri na hususan Bw. Spika, Naibu wake na Kamati yake ya Maspika. Pia nachukua nafasi hii kuwashukuru wafanyikazi wote wa Bunge la Kumi ambao tulishirikiana uzuri hata operators wa upande wa simu na wengineo wote. Naomba ya kwamba – kwa vile Baraza la Mawaziri bado linafanya kazi - lipitishe hoja ambayo iko kwenye Baraza lao kuhusu maswala ya pesa za wazee wa East African Community (EAC) ambao wameteseka kwa miaka 34. Mpaka leo, hawajapewa pesa zao. Naomba Baraza la Mawaziri lipitishe huo mswada kwa haraka kabla Baraza lao halijavunjwa ili wazee hao wa EAC ambao wameteseka kwa miaka 34 wapewe haki yao. Wenzao wa Uganda na Tanzania wamepewa haki yao. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia ningeomba Wizara ya Labour ifikirie na kuwalipa haki zao wafanyikazi wa African Safari Club walioko Shanzu, Mombasa. Na wao wapewe haki zao kwa haraka. Nafurahia kwamba mimi ni mmoja kati ya Wabunge wa Bunge la Kumi waliojaaliwa kupitisha Katiba mpya. Nawashukuru Wabunge wenzangu wote na ni jambo ambalo tutalikumbuka kwa miaka mingi. Pia, ningependa Wizara ya Ardhi itekeleze yale matakwa yalioelezwa katika Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Ardhi kuhusu ardhi za Lamu. Hususan, wale ambao walichukua ardhi kwa njia za haramu, wapokonywe hati zao na Wizara iweze kuangalia wale ambao walizaliwa pale ili wapewe haki yao. Ningewaomba Wakenya wote – kwa vile huu ni mwaka wa kwenda kupiga kura - tuhakikishe ya kwamba tumeweka amani. Tusisahau yale ambayo yalitufika mwaka wa 2007/2008; yasirejee tena. Yawe ni mambo ambayo Kenya hatutayaona wala kuyasikia tena. Hayo yatawezekana ikiwa Wakenya wenyewe wataweka amani na watakwenda kwenya kura na kampeni zetu bila chuki, bila ya kutukanana na bila kuleta ubaguzi wa rangi au ukabila. Pia, ningeomba kitengo cha polisi kikisaidiana na Wapwani kuangalia mambo ya Tana River. Hata jana tulipata habari ya kwamba katika Tana River, Wakenya 11 wameuliwa. Hili ni jambo ambalo tungependa kitengo cha polisi na Wizara inayohusika kufuatilia kwa haraka. Wenzetu Wakenya wanaoishi Eastleigh wanasumbuliwa mara kwa mara. Ni Wasomali lakini ni Wakenya. Tungetaka Wizara inayohusika iangalie Wakenya wanaoishi Eastleigh kwenye maswala ya biashara zao, waishi kwa amani. Wasisumbuliwe ili waweze kuendelea na kazi wanazozifanya kama Wakenya wengine. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}