GET /api/v0.1/hansard/entries/349245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 349245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/349245/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Lands",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": " Nashukuru, Bw. Naibu wa Spika, kwa kupata nafasi hii ili niweze kuwashukuru watu wa Kinango kwa kuniweka katika Bunge hili sasa nikitimiza miaka 15. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu, nikisema asante kwa yale ambayo niliweza kuyafanya kwa kipindi hicho. Ni imani yangu kwamba niliyafanya kwa uwezo wake Mola. Tunapokwenda kufanya sasa, maombi yangu ni kwamba Wakenya waiombee nchi hii kwa sababu uchaguzi unafuata si wa kawaida; na kwamba yale yatakayoipata umma tarehe 4.3.2023 tumeze kuyapokea kwa mikono miwili tukiwa na imani kwamba yote yatakuwa kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Sisi kazi yetu ni kuomba. Analoitikia Mwenyezi Mungu ndilo litakalo kuwa. Kwa hivyo kwetu ni kumuregeshea Mwenyezi Mungu ahsante. Miaka mitano ni muda mrefu. Kwa sababu bado ninavuta pumzi za uhai, ninamatumaini kwamba tarehe 4.3.2013 nitakuwa kwenye kinyang’anyiro ili kuangalia hatima ya maisha yangu ya kisiasa."
}