GET /api/v0.1/hansard/entries/34963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 34963,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/34963/?format=api",
"text_counter": 366,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Namshukuru Waziri kwa Mswada huu alioleta hapa ambao ni kuhusu vyama vya kisiasa. Jambo la kwanza, ninashukuru kwa sababu msajili wa vyama ataweza kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu, hata akipigiwa simu na kuambiwa kwamba kwa sababu chama fulani kiko karibu kushinda uchaguzi aandikishe chama kingine ili kukipinga hicho, hataweza kufanya hivyo. Ataweza kufanya kazi na usawa kwa Wakenya wote. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna baadhi ya watu ambao wanaunda vyama vya kisiasa kwa minajili ya kupata pesa kutoka nchi za nje. Madhumuni yao ni kupata utajiri. Watu wengi huunda vyama ili wakati wa uchanguzi waweze kuwauzia wanasiasa vyeti ili wachanguliwe. Mambo haya yote yatafika kikomo chake tukipitisha Mswada huu. Watu watakoma kuanzisha vyama vya kisiasa ili wapate utajiri. Kuna baadhi ya watu ambao hutafuta pesa nje ya nchi hii ili kuwachochea wananchi kuanzisha fujo. Jambo hili halitawezekana tena kwa sababu kila mtu atahitajika kuonyesha jinsi alivyopata pesa na vile atatumia pesa hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu utaweka msingi thabiti wa demokrasia yetu. Sheria hii itapiga vita vyama vya kikabila na kuhakikisha kuwa vyama vya kitaifa vimepata nguvu. Ningewaomba waheshimiwa Wabunge kuupitishe Mswada huu mara moja ili tuwe na umoja wa kisiasa hapa nchini. Muungano wa vya ni muhimu lakini tuungane kama Wakenya na si kama jamii hii na ile. Ni lazima kila chama kiwe na wafuasi katika county zote 47. Ikiwa vyama hivi vitakuwa na wafuasi kutoka kila pembe ya nchi, basi utaifa wetu utaimarika. Sisi tunataka kuona vyama ambavyo vitachangia pakubwa utaifa na uzalendo wa wananchi wetu."
}