GET /api/v0.1/hansard/entries/34964/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 34964,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/34964/?format=api",
"text_counter": 367,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, usajili wa vyama ni lazime uangaliwe kwa makini sana. Hatutaki kuona wafuasi wetu wakijiandikisha zaidi ya mara moja. Kuna baadhi ya watu ambao hupenda kujiandikisha mara kadha wa kadha katika vyama tofauti. Ni lazima uwanachama utiliwe maanani kwa sababu hatutaki mchezo wa paka na panya hapa. Kuna mtu ambaye asubuhi huwa mwanachama wa chama fulani, adhuhuri yuko katika chama kingine na jioni anajiandikisha kuwa mfuasi wa chama kingine. Huu ni mchezo ambao unatilia shaka misingi yetu ya kidemokrasia. Ni lazima tuhifadhi heshima yetu ikiwa tunataka kuheshimiwa na mataifa mengine ulimwenguni. Bw. Naibu Spika wa Muda, siasa zetu zimejikita katika miungano ya kikabila. Tunataka jamii za kutoka upande huu ziungane ili waweze kuunda Serikali baada ya uchaguzi ujao. Je, tukifanya hivyo, jamii zingine zitakwenda wapi? Hatutaki muungano unayoundwa katika misingi ya kikabila. Tunataka muungano wa vyama vya kitaifa. Muungano wa makabila ni hatari sana na utaleta utengano katika nchi hii. Kenya ni taifa moja. Lugha ya Kiswahili itiliwe mkazo sana kwa sababu inaweza kutuunganisha sisi sote. Wananchi wetu wanaielewa lugha hii vizuri sana. Ikiwa viongozi wote watatumia lugha hii, basi tutakuwa na taifa thabiti ambapo ukabila utapigwa vita. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}