GET /api/v0.1/hansard/entries/350727/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 350727,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/350727/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County Women Representative",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Bw. Spika, ajenda ya kwanza ni ardhi. Mheshimiwa Rais alisema kwamba ardhi ni katika vigezo ambavyo vinaleta mapato, ama kwa Kiingereza factor of production. Mimi nasema ardhi si tena kigezo cha kuweza kuzalisha. Ardhi ni kitu ambacho kimeleta tetesi na vita katika Jamhuri yetu ya Kenya, tukiangalia Rift Valley, ama Bonde la Ufa, na Pwani. Sasa hivi pia tunashukuru ndugu zetu wa kutoka Mkoa wa Kati na Bonde la Ufa. Walipiga kura pamoja. Hivyo basi, hakuna tetesi nyingi na shida ambazo tumeziona. Tunashukuru Mwenyezi Mungu lakini kitu ambacho tunasema ni kwamba, ni lazima viongozi tuwe wa kweli. Tulikuwa na tume ambayo ilituletea ripoti ya Ndungâu; pia tuna Tume ya TJRC ambayo ni ya kuleta ukweli, haki na maridhiano. Tume hizi zote zimetupatia ripoti na zikatueleza madhambi na mambo ambayo yamefanyika kuhusiana na mashamba; ajabu ni kwamba Ndungâu Report inaoza katika makabati ya Serikali. Jambo hili pia limezungumuziwa na tume ya ukweli na maridhiano. Je, hii tume ya ardhi itaweza kupatiwa nguvu za kisiasa na tutaweza kuwa Wakenya wa dhati ili Wakenya ambao ni maskwota, Wakenya ambao ni wakimbizi wa ndani, ambao tunawaita IDPs, waweze kupata mashamba?"
}