GET /api/v0.1/hansard/entries/350728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 350728,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/350728/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County Women Representative",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Katika Katiba yetu, sura ya tano inazungumzia swala la ardhi; inasema kuna ardhi ya kiserikali, ardhi ya kijamii na ardhi ya watu binafsi; katika mapendekezo mengi yalitolewa ni kwamba katika ardhi za kibinafsi viongozi wengi, tukiwemo sisi wa kisiasa, tumenyakua ardhi ya kiserikali. Tumenyakua ardhi za kijamii. Ni wakati wetu sisi kuwa mbele katika kuregesha ardhi hizo hata kama tuko katika nafasi kuu katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tuwe wa ukweli katika swala la ardhi. Tunataka akina mama tupate haki zetu za kumiliki ardhi na najua katika Miswada mitatu ambayo imetolewa na ile tume ya ardhi itaweza kufanya kazi; hii inamaanisha sisi viongozi tuwe wa ukweli."
}