GET /api/v0.1/hansard/entries/350880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 350880,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/350880/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "The Member for Saboti",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nakushukuru na kuwapongeza nyinyi wawili â wewe na Mhe. Spika â kwa kupewa wadhifa au nafasi mpya ambayo mlipata. Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza watu wa eneo Bunge la Saboti kwa kunichagua ili niwaakilishe kwenye Bunge hili. Nikichangia Hotuba ya Rais, ninajua kwamba ana nia nzuri. Hotuba yake ilikuwa nzuri sana na itakamilika iwapo itatekelezwa. Kwenye Hotuba yake, Rais aligusia masuala mengi ambayo yanaweza kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi hii. Hata hivyo, mambo hayo yote hayawezi kuwa iwapo hali ya usalama humu nchini haitaimarika. Ukitembelea sehemu zote za nchi hii, hakuna mahali ambapo hutosikia kilio juu ya ukosefu wa usalama. Hatuwezi kuzungumzia suala la usalama bila ya kuzungumzia mazingara ya walinda usalama wetu. Nimesema hivyo nikimaanisha kwamba kuna sehemu kadhaa humu nchi ambako mazingira ya walinda usalama wetu hayafai. Kwa hivyo, itakuwa vizuri sana iwapo suala hili litaangaziwa."
}