GET /api/v0.1/hansard/entries/350881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 350881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/350881/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "The Member for Saboti",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Sisi, wakazi wa Trans Nzoia, tunajivunia sana kilimo, na itakuwa vizuri sana iwapo masuala ya wakulima yataangaziwa. Kila kunapofika wakati wa musimu wa mvua, vifaa vya kilimo, na haswa mbolea, ambayo huletwa nchini kutoka ngâambo, vinakosekana. Itakuwa vizuri sana tukijiandaa mapema na vifaa vya kilimo ndiyo wakati wa kulima unapowadia wakulima wasihangaike kutafuta vifaa hivyo. Kwa mfano, mahindi hukuzwa Trans Nzoia lakini wakati wa upanzi ukiwadia, utaona kwamba hata mbegu za mahindi hazipatikani. Pia, bei ya mbegu huongezeka wakati huo."
}