GET /api/v0.1/hansard/entries/351445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 351445,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/351445/?format=api",
    "text_counter": 438,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon.Wario",
    "speaker_title": "April 17, 2013 PARLIAMENTARY DEBATES 37 The Member for Bura",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Bi Naibu Spika, ningependa kumshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa mwakilishi wa watu wa Bura. Nachukua nafasi niseme kongole kwako na pia kwa Spika wa Bunge, Rais na Naibu wa Rais mliochaguliwa katika nyadhifa mpya katika nchi ya Kenya. Nikizungumzia juu ya Hotuba ya Rais inaotoa mwangaza juu ya sera ya Serikali yake, Rais amegusia swala la ufisadi na uwazi. Kama Bunge tuna furaha kumuunga mkono kumsaidia kupambana na ufisadi. Swali ni kwamba, vipi tutafaulu katika hivi vita? Mashirika ambayo si ya kiserikali na ya kiserikali yameungana mkono kudhalilisha waajibu wa Bunge katika nchi ya Kenya. Iwapo Bunge haliwezi kufanya kazi yake ya kuchunguza rasilimali ya Serikali inavyotumika, vipi tutapambana na kushinda ufisadi? Hili ni swali kwake. Ninafuraha kwamba Rais amezungumzia ugatuzi. Ninajua kuna dukuduku juu ya magavana wanaotaka bendera, ofisi kubwa na pesa nyingi. Lakini watu wetu wako katika hali mbaya. Kumenyesha mvua ya gharika na magavana wetu hawana mikakati, sera, sheria ama maono juu ya vipi wataendeleza kazi na kuboresha hali ya maisha ya watu wetu. Kila kukicha ni bendera na wanataka ofisi kubwa kubwa. Tunazungumzia karakana kwa sababu katika Hotuba ya Rais alisema kwamba ataboresha karakana. Kati ya Bura na Garissa, zaidi ya magari 100 yamelala siku 20 njiani. Kama kweli mtaboresha karakana, halahala boresheni hali ya barabara inayounganisha Mombasa na Garissa. Nina furaha wakati Rais anazungumzia nafasi ya kazi kwa vijana. Kwa nini nina furaha? Asilimia 70 ya watoto wa Kenya licha ya kufanya vizuri katika vyuo vikuu, ajira ndilo tatizo kubwa. Mazungumzo yale yananifurahisha sana. Namwambia Rais kwamba haya mazungumzo yakifika ofisini, utekelezaji utakuwa ni tatizo kubwa. Nitamuunga mkono lakini atupe hakikisho. Katika Hotuba yake, Rais hakuzungumza juu ya janga linaloadhiri Wakenya; hili janga la kiasili likiwemo mvua ya gharika inayoendelea sasa. Ni lazima Serikali iwe na mikakati maalum. Ni lazima Serikali iwe na rasilimali maalum. Ni lazima Serikali iwe na mfuko ambao kutakapo tokea dharura itakimbia mara moja kuokoa watu. Angalia hali ya Mororo leo katika sehemu ninayowakilisha. Angalia hali ya Madogo na Bilbil. Ukame umefagia miji, watu hawana chakula na makao. Ukienda ofisini unaambiwa rudi siku nyingine maana wanalishughilikia tatizo lako. Hio siku itafika lini? Rais pia alizungumzia kawi. Tangu Mungu aumbe dunia na akamleta mtume Adam, mji wa Bangal haujapata stima. Nina furaha kusikia kutaletwa kawi ya solar lakini tangu Mungu kuumba dunia mji wa Bangal haujakuwa na umeme hata siku moja. Hii ni habari nataka kumpa Rais wangu atembee Bangal ajionee mwenyewe kwamba tangu Mungu aumbe dunia hata siku moja stima haijawaka kule. Nikimaliza, nina furaha kwamba Rais aligusia swala la elimu. Ningemwomba asome"
}