GET /api/v0.1/hansard/entries/352079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 352079,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352079/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Spika, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Tukizingatia umuhimu wa Kamati hii na umuhimu wa kuwa na Baraza la Mawaziri wakati unaofaa, sioni kama inafaa hata kwa mmoja wetu kusimama kupinga Hoja hii. Hata kama ingewezekana ingekuwa pengine watu wawili tu wazungumze kuhusu Hoja hii ili tuipitishe; inafaa tutoe nafasi kwa haraka kwa Baraza ili mawaziri wateuliwa katika wakati unaofaa. Mhe. Spika, katika wizara zilizobuniwa ni kama kuna vitengo vingine ambavyo vimeachwa nje. Mfano ni kitengo kile cha jinsia. Haijajulikana kitakuwa katika Wizara gani. Hivyo basi, inafaa kamati hii ijitwike wadhifa wa kuweza kuwashauri viongozi wahusika, Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa naibu wake, ili kitengo cha jinsia kiwekwe katika Wizara ambayo itatekeleza majukumu kama vile ilivyokuwa katika siku za nyuma. Mhe. Spika, pia katika harakati hizo za kubuni Baraza la Mawaziri, ningeuliza tena wahusika waangalie maeneo yote ya nchi ili yapate kuwakilishwa katika Baraza hilo. Hiyo itawafurahisha wananchi wa Jamhuri ya Kenya; wataona kwamba kila sehemu inawakilishwa katika Baraza hilo. Mhe. Spika, nina mengi lakini kufikia hapo nasema ninaunga mkono kwamba Hoja hii ipitishwe pasipo kusitasita. Asante Mhe. Spika."
}