GET /api/v0.1/hansard/entries/352168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 352168,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352168/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia County Women Representative",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 769,
"legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
"slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
},
"content": "Kulingana na ile Hotuba ya Rais, nasema hongera. Ilikuwa Hotuba nzuri sana lakini nataka tupige hatua katika mambo ya ulinzi na usalama katika sehemu ambayo nimetoka. Kabla zijasema hivyo, ningependa kutoa hongera kwa watu wa Laikipia kwa kuchagua huyu mama ambaye anaitwa Jane Machira. Niliapa mbele ya Bunge hili kwamba nitawatumikia wote. Tukiangazia ulinzi na usalama, Kenya ilifanya vizuri sana wakati ilielekea Somalia na kuhakikisha amani katika nchi hiyo. Lakini sisi wenyewe tunaweza kuwa tunakunywa maji, ili hali majirani wetu wanakunywa pombe za kifahari. Katika sehemu ya Laikipia, majirani wetu wamekuwa wakipigwa na kukipigana wenyewe kwa wenyewe na hata kuuana kwa ajili ya mifugo. Juzi tu, katika sehemu ya Kamwenje huko Laikipia, baba mmoja na mtoto walipoteza maisha yao. Pia katika Kaunti ya Baringo, ambayo ni jirani yetu, ilipoteza mtu mmoja na kijana wa shule. Pole kwa hayo yote. Mungu aweke roho zao mapahali pema peponi. Nataja tupige hatua ambayo Rais alizungumzia kuhusu ulinzi. Hatua ya kwanza inahusu watu ambao wameuliwa. Itakuwaje ikiwa jamii zao hawatapatiwa ridhaa? Tunataka watu hao wawe wakipatiwa ridhaa kwa sababu ikiwa mama amewachwa bila mzee wake na watoto bado wanasoma, anapata shida kubwa sana katika maisha yake. Kwa hivyo, katika Bunge hili, tungetenga kiazi fulani cha fedha za kuwalipa ridhaa waliofiwa na kuwa wajane. Tukiwa bado katika masuala ya ulinzi na usalama, kuna wazee ambao wanafanya kazi ya uhusiano mwema na kulinda usalama katika sehemu Fulani fulani. Tunawaamini sana. Lingekuwa ni jambo la busara kuwatengea fedha kidogo za malipo. Tunawaita wazee wa mitaani, na wanasaidia jamii zinazoishi Laikipia. Jambo la tatu, ni kuwa kuna tatizo la wanyama wa pori kuzurura huko Laikipia. Hao wanyama wa pori wemawatatiza wananchi wa Laikipia. Watoto wetu siyo kama"
}