GET /api/v0.1/hansard/entries/352241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 352241,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352241/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Aburi",
"speaker_title": "The Member for Tigania East",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": " Mhe. Spika, mimi ni Mheshimiwa aliyeshindwa mara saba na ya nane akachaguliwa kuja hapa ndani. Natoa shukrani kubwa sana kwa wewe kupata hicho kiti. Najua wewe ni kiongozi ambaye atatuongoza tukiwa pamoja. Natoa pia shukrani kwa Mwenyezi Mungu kunileta hapa na watu wa Tigania Mashariki. Pia nimekutana na ndugu yangu Mhe. Kabando wa Kabando tuliyekuwa naye 1992 na Mhe. Chris Bichage ambaye pia tulikuwa naye tukipigania haki. Kutoka wakati huo, sijawahi kupumzika hadi sasa niko Bunge. Kwa hivyo, nasema ahsante kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu wa Tigania Mashariki kwa kunileta Bungeni. Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri sana. Sisi watu wa Upinzani wa chama cha ODM hatufai kuwa tunapingana na kila kitu. Saa zingine tuseme kingine ni kizuri. Hotuba ya Rais aliyoisoma katika Bunge hili ilikuwa nzuri sana. Ukiingia Tigania Mashariki, kuna mahali panaitwa Amgaa, Ngutu na Kunati. Ukiingia zaidi magharibi sehemu ya Ndia, barabara imekatika na hakuna daraja. Zile shule ambazo zitapelekewa laptops, mahali pengine watoto wanasomea chini ya miti. Hivi sasa, ukimpelekea mtoto laptop akiwa chini ya mti na mvua inyeshe, laptop hiyo itaharibika. Kwanza, tunataka shule zijengwe halafu laptops zifuate. Katika sehemu ya Tigania Mashariki, hakuna hospitali ilihali inapakana na Igembe ya Kati na Igembe Kusini. Watu wa Tigania Kusini wa kutoka upande wa Ngutu na wale wanaotoka Kunati wana hospitali. Lakini sisi hatuna chochote. Inaonekana ni mahali hapawezi kupata uhuru lakini kwa sababu Mhe. Kenyatta amepata Serikali na watu wa Tigania Mashariki walimpigia kura na kunipigia mimi, ni lazima afike kule aone wale ni wazalendo Waafrika awapiganie. Hawa ni wazalendo wa Afrika ambao walipigania uhuru na wakapata. Ningependa kuzungumzia masuala yanayohusu kahawa. Eneo letu la Tigania Mashariki lilikuwa nambari moja katika kilimo cha kahawa. Lakini kahawa iliharibiwa na ikachafuka. Wakulima wa eneo la Tigania Mashariki walingâoa kahawa wakapanda"
}