GET /api/v0.1/hansard/entries/352246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 352246,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352246/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wangu napewa Kshs300,000 ama ni Kshs500,000!” Nikamwambia: “Hizo ni pesa nyingi sana! Akaniambia: “Ngoja kidogo tuone Mhe. Aburi.” Tulikaa katika kanisa na wakati kasisi alipomaliza misa yake, yule mtu aliyekuwa anapingana na yeye aliamka na kutoa Kshs100,000. Akaniambia: “Aburi, nitafanya nini kwa sababu watu wote katika kanisa hili wanangoja kuona mheshimiwa atatoa pesa ngapi? Kwa sababu mheshimiwa asipotoa pesa, hawawezi kuamka na kupiga makofi.” Wakati huu katika mashinani, anayeangaliwa atatoa ngapi ni mheshimiwa. Mheshimiwa amekuwa maskini katika Bunge hili na waliomchagua wanampigia simu za kuomba pesa, simu za kuarifu kifo na za kuomba pesa za kujenga makanisa. Mheshimiwa asipotoa pesa, hapigiwi makofi. Nasema hivi: Lazima tuungane pamjoa – tukiwa wanachama wa ODM, PNU ama vyama vingine - katika vita hivi hadi tufike mwisho. Jambo langu lingine ni hili: Nawalaani wale wazee wa Njuri Ncheke waliomtukana Mheshimiwa Mithika Linturi. Mheshimiwa Mithika Linturi ni mbunge ambaye tunamwamini katikia Bunge hili. Anapigania Mkenya na kila mtu. Wale hawakuwa wazee wa Njuri Ncheke ! Wazee wa Njuri Ncheke w anamwita mtu katika nyumba ya Njuri Ncheke na kuongea pamoja na kumaliza mambo yao. Siyo mambo ya kwenda kwa magazeti na kusema: “Huyu ni mtu mbaya!” Mhe. Spika, yangu hayajaisha! Ya Mpuru Aburi hayajaisha! Lingine ni hili. Tunaenda kukutana na wabunge wa Tigania Mashariki; Igembe, Ntonyiri na upande wa Thuci. Tutaenda kukutana katika nyumba na Njuri Ncheke na kuwalaani wale wazee ambao walioongea vibaya kuhusu wabunge wa Meru. Walisema ya kwamba ni wakora wasioshiba. Wanafaa kuongezewa kokoto kwa tumbo---"
}